Wednesday, October 7, 2015

UNAWEZA KUTOKA HIVI??

Moja kati ya vitu ambavyo vinateka nyoyo za wadada wengi ..kwa karne hii ya sasa ni denim shirts (shati lenye muonekano wa jinzi) ...hasa ukiipatia kuivalia na accessories zenye mvuto..kama mrembo huyu ..
Kiukweli amenoga√√

Friday, October 2, 2015

Kimya kingi

SABABU YA KUWA KIMYA

Natumai umzima wa afya ewe msomaji wa safu hii ya urembo ,naomba niombe radhi kwa ukimya wa mda mrefu ulio weza kufanya kazi na nguvu ya kuendesha safu hii kupunguza ufanyaji kasi yake ya kazi , yote ni kutokana na kuomboleza msiba wa baba yangu kipenzi uliotokea 9/2/2015 ..
  Kwasababu yote ni kazi Ya mungu hivyo sina budi kumshukuru kwa kila jambo na kumuomba nguvu Mpya ya kunifanya Mimi kuweza kushiriki vyema katika safu hii ..KARIBU....

Sunday, October 26, 2014

PENCIL SKIRT

Mnamo  miaka   ya  1940   mwana mashuhuri  mkongwe    katika   maswala   ya  fashion  nchini   ufaransa aliyejulikana   kama    Christian dior  aliweza   kubuni  muonekano huu  wa  skirt  aina  ya  pencil , muonekano   huu  wa sketi  ni  wakipekee  huweza  kumpa  mtu  fursa  ya  kuchagua  ni  mahala  gani  anaweza  kutoka  na  muonekano  huu ,  iwe  kwenye  party  ,  ofisini  ,  hata  casual  pia   inakua  ni  vizuri  maana   umfanya   mtu  kuonekana  na  na  mvuto  bomba   pasipo   kuchagua    umbo   la   mtu   maana  mtu   mwenye  umbo   la   aina   yeyote    upendezwa   nayo    .  

        PENCIL   SKIRT'S

WEDGES

Wengi  wetu  tumezoea  kuona viatu  mbali mbali  pasipo  kujua  aina  ya  viatu  hivyo,  hebu  leo  tutizame  viatu  hivi  viitwavyo  wedgese , 
Viatu  hivi  ni  moja  kati  ya  viatu  pendwa  sana  na  wadada  kwasababu  kuu  moja ,  viatu  hivi  umfanya  mtu awe  na uwezo  wa  kuvitembelea  tofauti  na  viatu  vya  mchuchumio  au  vimezoeleka  kuitwa   high  heels ,
Pia viatu  hivi navyo vimegawanyika  katika  miundo  tofauti  tofauti   kama  vile   sniker wedges   na   boot wedges ,   hivi  apa  ni  mfano  wa  snikers  wedges  pamoja  na  wedges  .

SNIKER'S   WEDGES    NA  WDGES   ZENYEWE

Tuesday, October 21, 2014

Wednesday, October 15, 2014

MAKENZE

Makenze  , hiki  kitenge  kimeweza  kuteka  nyoyo  za  watu  wengi  sio  kwa   wanawake  tu  bali  hata  kwa  wanaume  , 
Unaweza  kuchagua  mshono  wowote  unaohisi  utavutiwa   nao  nakupata  muonekano  bomba.

Sunday, October 12, 2014

Miss Tanzania

Picha ya  pamoja

Mshindi  wa  Redd's  miss Tanzania  Sitti  Abbas  Mtemvu  katikati  , na  mshindi  wa  pili Lilian kamazima (kulia) , akifuatiwa  na  mshindi  wa  tatu  Jihan Dimanhk (kushoto)