Sunday, October 26, 2014

PENCIL SKIRT

Mnamo  miaka   ya  1940   mwana mashuhuri  mkongwe    katika   maswala   ya  fashion  nchini   ufaransa aliyejulikana   kama    Christian dior  aliweza   kubuni  muonekano huu  wa  skirt  aina  ya  pencil , muonekano   huu  wa sketi  ni  wakipekee  huweza  kumpa  mtu  fursa  ya  kuchagua  ni  mahala  gani  anaweza  kutoka  na  muonekano  huu ,  iwe  kwenye  party  ,  ofisini  ,  hata  casual  pia   inakua  ni  vizuri  maana   umfanya   mtu  kuonekana  na  na  mvuto  bomba   pasipo   kuchagua    umbo   la   mtu   maana  mtu   mwenye  umbo   la   aina   yeyote    upendezwa   nayo    .  

        PENCIL   SKIRT'S

WEDGES

Wengi  wetu  tumezoea  kuona viatu  mbali mbali  pasipo  kujua  aina  ya  viatu  hivyo,  hebu  leo  tutizame  viatu  hivi  viitwavyo  wedgese , 
Viatu  hivi  ni  moja  kati  ya  viatu  pendwa  sana  na  wadada  kwasababu  kuu  moja ,  viatu  hivi  umfanya  mtu awe  na uwezo  wa  kuvitembelea  tofauti  na  viatu  vya  mchuchumio  au  vimezoeleka  kuitwa   high  heels ,
Pia viatu  hivi navyo vimegawanyika  katika  miundo  tofauti  tofauti   kama  vile   sniker wedges   na   boot wedges ,   hivi  apa  ni  mfano  wa  snikers  wedges  pamoja  na  wedges  .

SNIKER'S   WEDGES    NA  WDGES   ZENYEWE

Tuesday, October 21, 2014

Wednesday, October 15, 2014

MAKENZE

Makenze  , hiki  kitenge  kimeweza  kuteka  nyoyo  za  watu  wengi  sio  kwa   wanawake  tu  bali  hata  kwa  wanaume  , 
Unaweza  kuchagua  mshono  wowote  unaohisi  utavutiwa   nao  nakupata  muonekano  bomba.

Sunday, October 12, 2014

Miss Tanzania

Picha ya  pamoja

Mshindi  wa  Redd's  miss Tanzania  Sitti  Abbas  Mtemvu  katikati  , na  mshindi  wa  pili Lilian kamazima (kulia) , akifuatiwa  na  mshindi  wa  tatu  Jihan Dimanhk (kushoto)

REDD'S MISS TANZANIA 2014

Sitti Abbas Mtemvu huyu  ni  mrembo  kutoka  wilaya  ya  Temeke,  
 Mrembo huyo  ambae  baba  yake ni  
mbunge  wa  Temeke  Mh. Abass Mtemvu ,  ameweza  kutwaa  taji  la  Redd's Miss Tanzania  2014.
Mashindano  hayo  ambayo  yalifanyika  ukumbi  wa  mlimani city  jijini  Dar es salaam  hapo  Jana.
Kutokana  na  ushindi  huo  ameweza  kuondoka  na  kiasi  cha  pesa  taslim  milioni  18  huku  akifuatiwa  na  mshindi    
wa  pili  ambae  aliondoka  na  kiasi  cha pesa  taslim  million   sita.
Mrembo  huyu  anakibarua  kikali  cha kuiwakilisha  Tanzania  katika   kuwania  miss world 2015  



VILEMBA

Monday, October 6, 2014

IJUE NGUO NYEUSI

Miongoni mwa walio  wengi upendelea kuvaa vazi hili kutokana na rangi yake kuonekana ni yakutuliza rangi Kali , na kufanya iyonekane vizuri machoni bila kuumiza macho .
Vazi lenye rangi nyeusi umuelezea mtu kwa namna yake  kana kwamba mtu akivaa rangi nyeusi anajielezea kua Yeye ni mtu jasiri , mwenye kujitambua na yupo makini wakati wote.
Vazi lenye rangi nyeusi  upendwa sana kuvaliwa sehemu za interview , night party au dinner , ata mchana pia endapo tu utaweza kuchanganya na rangi nyengine kidogo .
Kwa uhakika usio fikirika ni kwamba hautokua ukilitendea haki vazi hili endapo utalivaa mchana wakati wa  jua Kali , au kipindi cha joto maana rangi nyeusi na vitu hivi aviakisi tena ukiwa umevaa full black yani juu mbaka chini.

UMREMBO MODELS WAKIWA WAMEVALIA VAZI JEUSI NA MCHANGANYIKO WA RANGI NYENGINe:

UVAAJI WA NGUO NYEUSI

Sunday, October 5, 2014

CRAZY COLORS

Najua wengi wetu uwa  tunajikuta kwenye wakati  mgumu  pindi linapo kuja suala  la kupangilia  rangi sahihi ya vazi tunalo vaa, ama mchanganyiko  wa rangi tofauti tofauti.
Wengi wetu huaribu muonekano huu pindi tuanapo  kuwa hatuelewi ni rangi ipi ambayo itafaa kuendana na rangi nyengine.
Hebu leo nizungumzie nguo zenye muoneka wa rangi  kali ama zimezoeleka  kwa jina  la  crazy color

TIPS ZITAKAZO KUSAIDIA KATIKA    KUCHANGANYA RANGI

  1.Kwanza unatakiwa kufahamu rangi ipi ambayo itaenda kutawala katika vazi lako kama ni hot pink ,njano,blue ama zambarau.

2. Vile vile hiyo rangi inatakiwa iendane na vito ambavyo utaenda kuvaa  kama vile ,mkufu wenye rangi kali , hereni zenye rangi kali , pochi yenye rangi kali na viatu pia.

3. Makeup , katika kukamilisha muonekano wako wa makeup jaribu kupaka rangi zenye kuonekana kama vile,  wanja rangi ya zambarau na lip gloss yenye rangi ya hot pink.

4. Kua makini sana katika namba ya rangi ambazo utachanganya  itakua ni vizuri zaidi  kama  utachanganya
rangi kuanzia  tatu hadi nne , lakini endapo utachanganya rangi nyingi zaidi itakua ni kichekesho kwa mfano mchanganyiko wa rangi tano hadi kuendelea.

Endapo utazingatia hayo  haito kua shida katika kuchanganya rangi mbali mbali zenye muonekano mkali , na la muhimu zaidi ni kujua rangi yako ya mwili , kama ni mweusi sana basi ni bora uka punguza rangi ya nguo unazo enda kuchanganya , na kama ni mweupe unaweza ukatumia rangi zenye uwingi wowote.

  MFANO WA RANGI ZA NGUO ZINAZO VUTIA 

Monday, September 29, 2014

Wow MAX !!

Sketi ndefu aina ya max upendezea na muonekano simple wa top utakayo tupia  ,kuendana na rangi pia, ili usije  kuharibu muonekano huo hebu waone hawa warembo na   mpangilio walio match nao ,je  zina vutia ?

KABLA NA BAADA

Hiyo ni kabla na baada ya make up..muonekano huu ni wakawaida tu.unaweza kutoka nao sehemu yoyote ile

Wednesday, September 17, 2014

ABOUT UMREMBO;

Its all about fashion to ladies who want to try knew things in clothes,shoes,accessories,hair and make up its all about before and after you will get the time to see how a person looks before and after make up or wearing a designer clothes .I hope you will enjoy and start up new thing about fashion from me ,www.mwendastellah@gmail.com