Sunday, October 5, 2014

CRAZY COLORS

Najua wengi wetu uwa  tunajikuta kwenye wakati  mgumu  pindi linapo kuja suala  la kupangilia  rangi sahihi ya vazi tunalo vaa, ama mchanganyiko  wa rangi tofauti tofauti.
Wengi wetu huaribu muonekano huu pindi tuanapo  kuwa hatuelewi ni rangi ipi ambayo itafaa kuendana na rangi nyengine.
Hebu leo nizungumzie nguo zenye muoneka wa rangi  kali ama zimezoeleka  kwa jina  la  crazy color

TIPS ZITAKAZO KUSAIDIA KATIKA    KUCHANGANYA RANGI

  1.Kwanza unatakiwa kufahamu rangi ipi ambayo itaenda kutawala katika vazi lako kama ni hot pink ,njano,blue ama zambarau.

2. Vile vile hiyo rangi inatakiwa iendane na vito ambavyo utaenda kuvaa  kama vile ,mkufu wenye rangi kali , hereni zenye rangi kali , pochi yenye rangi kali na viatu pia.

3. Makeup , katika kukamilisha muonekano wako wa makeup jaribu kupaka rangi zenye kuonekana kama vile,  wanja rangi ya zambarau na lip gloss yenye rangi ya hot pink.

4. Kua makini sana katika namba ya rangi ambazo utachanganya  itakua ni vizuri zaidi  kama  utachanganya
rangi kuanzia  tatu hadi nne , lakini endapo utachanganya rangi nyingi zaidi itakua ni kichekesho kwa mfano mchanganyiko wa rangi tano hadi kuendelea.

Endapo utazingatia hayo  haito kua shida katika kuchanganya rangi mbali mbali zenye muonekano mkali , na la muhimu zaidi ni kujua rangi yako ya mwili , kama ni mweusi sana basi ni bora uka punguza rangi ya nguo unazo enda kuchanganya , na kama ni mweupe unaweza ukatumia rangi zenye uwingi wowote.

  MFANO WA RANGI ZA NGUO ZINAZO VUTIA 

No comments:

Post a Comment